Ruka hadi maudhui makuu
St Mary's Junior Seminary VisigaSeminari ya Visiga, Jimbo Kuu la Dar es Salaam

Kuhusu

Kuhusu Sisi

Seminari Ndogo ya Mtakatifu Maria ipo chini ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam imejikita katika kulea waseminari walio na wito wa upadri. Katika msingi wa imani, nidhamu, na ubora wa masomo, seminari hutoa elimu jumuishi inayowaandaa wanafunzi kiroho na kiakili kwa ajili ya wito wao.

Mpango wa maendeleo ya shule

Dira ya Visiga Seminary

Dira ya seminari ni kuandaa makuhani wa baadaye kwa ajili ya kanisa katoliki la jimbo kuu la Dar es Salaam na kwa ujumla kanisa zima.

Nanyi mtabaki kuwa mashahidi wangu

— Matendo 1:8

Dhamira ya Visiga Seminary

Dhamira ya seminari ni kutoa mafunzo yaliyokamilika: Kiroho, kielimu, binadamu na kipastorali kwa wanafunzi wa seminari.

Mafanikio na Malengo

Kwa miaka 30 iliyopita seminari imeweza kuwa na makuhani wengi waliosoma Visiga Seminary. Kwa miaka 25 ijayo tunapanga kuwa na zaidi ya makuhani 90 baada ya kuanzisha elimu ya sekondari ya kidato cha tano na sita.

Kauli mbiu

Sala, masomo, kazi na nidhamu, ambavyo vitachangia kufikia mpango wa maendeleo ya seminari.